Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kufuatia matusi ya Rais wa Marekani, Donald Trump, dhidi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Issa Qassim, kiongozi wa kiroho wa Mashia wa Bahrain, alitoa tamko ambalo maandishi yake ni kama ifuatavyo:
Ni wazi kwa kila mtu kuwa dunia ya leo, miongoni mwa idadi kubwa ya mataifa na serikali—iwe ni zile zinazopingana na Marekani au zile zinazohesabiwa kuwa marafiki wake—imekumbwa na hofu kubwa kuhusu hatima yao na hatima ya dunia nzima.
Ni hofu inayotokana na hatari ya jumla na yenye uharibifu mkubwa, hali ambayo ndani yake haisikiki sauti yoyote isipokuwa sauti ya nguvu ya kimaada isiyozuilika, huku akili, dini, maadili na mantiki ya maumbile tukufu ya mwanadamu vikikosekana kabisa. Chanzo kikuu cha hofu hii iliyoenea duniani ni sera zisizodhibitiwa za Rais wa Marekani na mwelekeo wake wa uharibifu wa pande zote kwa ajili ya kutimiza utawala wa kidhalimu wa kibeberu duniani.
Katika muktadha huu, swali linaibuka kuhusu aina ya “marekebisho” ambayo Trump anadai kuwa ni wajibu kuyaweka juu ya uongozi wa juu wa Jamhuri ya Kiislamu! Uongozi ambao una sifa za ukamilifu zilizofanya maandamano ya mamilioni ya watu yajaze barabara za jamhuri hii iliyobarikiwa, kwa ajili ya kuuunga mkono dhidi ya harakati za kihujuma na chuki; harakati ambazo adui alizifadhili, akazilea na kutangaza uungaji mkono wake waziwazi, hadi kufikia kuingilia moja kwa moja mfumo rasmi wa dola, kwa lengo la wakati ufaao na bila kuchelewa, kuikandamiza jamii, mali, miundombinu na kila kitu ambacho maisha ya watu yanategemea, ili kuangamiza Jamhuri ya Kiislamu kabisa bila kuacha nafasi yoyote ya kurejea kwake.
Je, hata Muirani mmoja mwenye akili timamu anaweza kuamini kuwa uvamizi wa kijeshi wa kikatili wa Marekani na Israel katika vita vya siku kumi na mbili, pamoja na juhudi zilizofuata za kuwasha vita vya moja kwa moja vilivyo vikali zaidi, vikubwa zaidi, vyenye uharibifu na umwagaji damu zaidi, unatokana na huruma ya Trump na heshima au kujali kwake maslahi ya wananchi wa Iran, uhuru wao, kujitawala kwao na heshima yao?
Ayatullah Khamenei ni shakhsia iliyofikia kilele cha juu kabisa katika nyanja za kielimu, kiroho na kisiasa; ni kiongozi mwenye sifa za kipekee anayeng’ara miongoni mwa viongozi wote duniani leo.
Ni kiongozi ambaye mamilioni ya wanaume na wanawake mashuhuri nchini Iran wako tayari kuyatoa maisha yao kwa ajili yake, wanauona uamuzi wake kuwa ni uamuzi wa dini ambao hairuhusiwi kuupinga, na wanauona usalama wake kuwa ni sehemu ya usalama wa Uislamu na Umma.
Ni kiongozi ambaye anaungwa mkono na umma mpana uliosambaa kote duniani; umma ambao uko tayari kuyatoa maisha yake kwa ajili ya usalama wake na kwa ajili ya kuendelea kwa baraka zake katika Umma wa Kiislamu na jamii tukufu ya wanadamu kwa ujumla.
Faida ya uwepo wa uongozi huu ni manufaa ya jumla kwa kila mwanadamu mwenye heshima na uadilifu; na kauli yake, mchango wake na jihadi yake ni kwa ajili ya usalama, amani, kheri, ustawi na undugu duniani kote.
Maoni yako